YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Sample

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

DAY 1 OF 31

Tunapoanza mwaka mpya ni muhimu sana tukajiwekea malengo. Biblia haikatazi kufanya hivyo, mradi tumshirikishe Mungu katika mipango yetu ili atuongoze katika yote, kwani sisi hatujui kesho itakuwaje, lakini yeye anajua. Hatima ya maisha yetu iko mikononi mwake. Lengo letu kuu liwe kuutafuta kwanza ufalme wake na haki yake, naye ameahidi kutuongoza na kutubariki. Alivyoandika Yakobo, baraka hizi zitakuwa pamoja na kujua kutenda mema na kulindwa dhidi ya majivuno.

Scripture

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More