YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Sample

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

DAY 2 OF 31

Sikukuu ya Epifania ina habari njema kwetu: Nuru yako imekuja. Yesu aliye nuru ya ulimwengu ametujilia. Tukitembea naye tutakuwa nuru ya ulimwengu, jinsi Mungu alivyokusudia. Ni kweli kwamba hali ya ulimwengu tunayoishi inazidi kuwa mbaya. Itakuwa mbaya zaidi tusipohubiri Injili, na watu wakamjua Mungu na kuacha maovu. Pale Injili itakapokubalika, hata hali ya uchumi itakuwa ya neema. Hivyo tuna kila sababu ya kufanya kazi ya Bwana kwa furaha na nguvu zaidi tukiongozwa na Roho Mtakatifu.

Scripture

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More