YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Sample

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

DAY 4 OF 31

Jina la huyo mtumishi ambaye Ibrahimu alimtuma ni Eliezeri (15:2). Alikuwa mcha Mungu kama Ibrahimu, na katika kutimiza wajibu wake alimtegemea Mungu. Hakujiamini mwenyewe kwamba ataweza kufanikiwa kwa uwezo wake (m.12-14, 26-27, Akasema, Ee Bwana, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, nakuomba mambo yangu uyajalie yawe heri leo, ukamfadhili bwana wangu Ibrahimu. ... Yule mtu akainama akamsujudu Bwana. Akasema, Na atukuzwe Bwana …)! Eliezeri alikuwa mtu wa maombi. Bila shaka ni jambo ambalo amejifunza kwa Ibrahimu mwenyewe! Ni dalili ya imani iliyo hai. Nasi tufuate mfano wake. Tusimtumikie Bwana kwa kutegemea nguvu zetu, bali kwa kumkabidhi yeye njia zetu! Zingatia hekima ya Sulemani anaposema, Mkabidhi Bwana kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika (Mit 16:3).

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More