YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

DAY 10 OF 30

Kila mtu atatiwa chumvi kwa moto (m.49). Chumvi ni neno la Yesu. Kwa kulisikia neno hilo mtu ataokoka, atampata Roho Mtakatifu moyoni mwake. Sasa kuokoka kunafanyika kwa moto, yaani kwa utakaso. Utakaso huu Roho Mtakatifu anaufanya kwa nguvu ya neno la Yesu, kama ombi la Yesu katika Yn 17:17 linavyoonyesha: Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. Mtu anapata uchungu moyoni mwake kutokana na dhambi zake. Anatambua kuwa amemkosea Mungu. Hali hii inamfanya atubu, akiziungama dhambi zake na kuziacha kwa Yesu. Ni maana ya habari za m.43-48 kuhusu kukata mkono na mguu, na kuling’oa jicho na kulitupa! Tutubu lile linaloifanya mikono yetu kutukosesha! Lazima tuishi maisha ya toba. Kwa sababu kila mtu atatiwa chumvi kwa moto. Chumvi ni njema; lakini chumvi ikiwa si chumvi tena, mtaitia nini ikolee? Mwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa ninyi (m.49-50).

Scripture

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More