YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

DAY 15 OF 30

Wanafunzi walikuwa wazito kusikia na kuelewa fundisho la Yesu kuhusu cheo katika ufalme wa Mungu. Wewe uliye na cheo fulani katika kanisa, je, umelielewa? Fundisho la Yesu ni kwamba ukuu katika ufalme wa Mungu ni kutumia cheo ulichopewa kwa ajili ya kuwahudumia na kuwatumikia wale unaowaongoza: Mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mtumishi wenu, na mtu anayetaka kuwa wa kwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote (m.43-44). Ukitumia nafasi yako kwa ajili ya kujikuza na kujinufaisha mwenyewe, hufai kuwa mtumishi wa Bwana! Yesu mwenyewe ni mfano kwako wa kufuata. Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi (m.45; ukiwa na nafasi, soma pia Flp 2:3-8). U heri ukitubu na kutii!

Scripture

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More