Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Siku 21 za KufurikaMfano

21 Days to Overflow

SIKU 21 YA 21

Uaminifu wa Mungu

Imani yetu lazima ifike mahali ambapo tunaaamini Mungu ana mambo makubwa kwa ajili yetu, na tuko tayari kuyaomba. Ili kufika mahali hapo yatupasa kutubu kila mawazo madogo. Wote tumehukumiwa nayo. Wote tunahukumiwa kwa kujaribu kubashiri muundo wa Mungu. Wote tumejaribu kuweka mkakati wa jinsi anavyoweza kutimiza jambo tulilomuomba. Mara nyingi, hafuati muundo tuliodhani angefuata. Ni kwa sababu mawazo yetu ni madogo.

Efeso 3:20, inaweka sahihi. “Yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo." Mungu anatosha. Pasipo kujali hali, pasipo kujali utupu, pasipo kujali ukiwa, pasipo kujali uhitaji, yeye anatosha. Na ni zaidi ya kutosha.

Lazima tujue mikate mitano na samaki wawili wanatosha sana kulisha maelfu. Lazima tujue kuzitweka nyavu zetu upande mwingine na mtumbwi kutatuletea samaki wengi tuliokuwa tunawatafuta usiku kucha. Lazima tufikirie sana na kumuomba Mungu atuoneshe ukubwa wake katika hali zetu na siyo kumuwekea mipaka katika uwezo wetu. Lazima tuondoke katika mawazo kwamba vitu lazima viwe kwa namna fulani. Njia zake ziko juu kuliko njia zetu; mawazo yake yako juu sana kuliko mawazo yetu. Kutembea katika ujazo, lazima tujiweke katika hali ya kupokea utimilifu wa Mungu. Ninakuahidi, itakuwa zaidi ya ambavyo uliwahi kufikiria itakuwa.

Kolosai 2:8-10 inatuonya tusifanywe mateka kwa elimu ya bure na madanganyo matupu. Hatuwezi kuruhusu kusahau kwamba tunamtumikia yeye ajuaye yote, awezaye yote, aliopo kila mahali, Bwana wa mbingu. Lazima tukatae mawazo madogo na tuwe wazi kwa mawazo makubwa, ya ajabu, mambo ya Mungu yasiyo ya kawaida anayotaka kuyafanya kupitia kwetu na maishani mwetu!

Huko ni kufurika. Hatuhitaji kujua kwa namna gani, lini, wapi, au itatokea kwa nani. Tunahitaji tu kumwamini Mungu kuweza kutimiza kwa ajili yetu na utukufu wake. Ni wakati wa kuacha mipango yetu. Tukifanya hivi, tutaona miujiza.

Ni wakati wa kutambua na kukumbatia ujazo, maisha yanayoongozwa na Roho ambayo Mungu amekusudia uishi. Ni wakati wa kufurika kwa utukufu wa Mungu!

Safari yako haiishii hapa. Hizi ni siku 21 tuu za safari yako ya kufurika. Sasa, chukua kanuni zilizoandikwa kuhusu mpango huu nakuzitumia katika maisha yako ya kila siku.

Una njaa zaidi? Angalia Jeremiah Hosford’s siku 21 za kufurika. Kitabu hiki inajadili siku 21 za mpango huu kwa undani zaidi na kukupa maelekezo zaidi kwa siku 22 na zaidi.

Kuhusu Mpango huu

21 Days to Overflow

Katika siku 21 za kufurika mpango wa YouVersion, Jeremiah Hosford atawachukua wasomaji safari ya majuma 3 ya kujimimina wao kwa wao, kujawa na Roho Mtakatifu, na kuacha mafuriko, na maisha yaliyojaa Roho. Ni wakati wa kuacha kuishi kawaida na kuanza kuishi maisha ya kufurika!

More

Tungependa Kuishukuru YouVersion kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya https://www.theartofleadership.com/