Siku 21 za KufurikaMfano

Ushirika na Roho Mtakatifu
Tumetumia juma zima kujimimina sisi kwa sisi. Tulitumia juma zima ili kujazwa na Roho Mtakatifu. Sasa, tunahama kutoka kushughulika na kinachoendelea ndani yetu kwenda katika kutembea katika kina cha kufurika. Ninaamini kwa imani kwamba tayari umeanza kuona mafuriko ya ajabu kutoka kwa Mungu.
Ili tuweze kutembea katika mafuriko, lazima tupite hatua ambapo kutembea kwa Roho Mtakatifu ndani yetu in tukio, na badala yake inakuwa ni mtindo wa maisha. Tunapofika mahali ambapo Roho anatutia moyo kila tunachokifanya, kusema, kufikiri, na kujisikia, tunatembea katika ushirika, na Roho Mtakatifu.
Hiki ndicho Paulo anachokisema wakati anafunga waraka wake wa pili kwa kanisa la Korintho (2 Wakorintho). Katika 2 Wakorintho 13:14, tunamuona Paulo akitamani kwamba neema ya Bwana Yesu Kristo, upendo wa Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nao. Na hakuwa anazungumza juu ya wakati wa ushirika na Roho --alikuwa akizungumza juu ya mtindo wa maisha.
Tunamuona Roho Mtakatifu kama mtindo wa maisha tofauti na tukio tena katika Yohana 14:16. Yesu anasema hapa kwamba atamuomba Baba Roho Mtakatifu ili akae nao "milele."
Itakuwaje kama tutaamka kila siku na lengo letu la kwanza ni ushirika na Roho Mtakatifu? Je maisha yetu yangekuwa na tofauti gani kama tungeanza siku zetu tukimuuliza anataka tufanye nini kwa siku aliyotupa? Uongozi wa Roho Mtakatifu ungetupeleka mahali ambapo hatukuwahi kuota tutafika na angeturuhusu kutimiza mambo ambayo hatukuwahi kufikiria kwamba tunaweza kutimiza. Roho Mtakatifu hutamani kuwa na ushirika, katika mazungumzo, katika mafunuo pamoja nasi kila siku. Anatamani kutuonesha vitu katika neno, katika maono, na katika ndoto.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Katika siku 21 za kufurika mpango wa YouVersion, Jeremiah Hosford atawachukua wasomaji safari ya majuma 3 ya kujimimina wao kwa wao, kujawa na Roho Mtakatifu, na kuacha mafuriko, na maisha yaliyojaa Roho. Ni wakati wa kuacha kuishi kawaida na kuanza kuishi maisha ya kufurika!
More