Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Siku 21 za KufurikaMfano

21 Days to Overflow

SIKU 1 YA 21

Ulimwengu

Tunaanza safari hii kwa kujimimina sisi kwa sisi. Biblia inatuambia, kama wafuasi wa Kristo, tulionunuliwa kwa damu ya Yesu, ambao tumejazwa na Roho, kwamba hatutakiwi kupenda vitu ya dunia hii. Najua hii ni tofauti kabisa na mambo mengi yanayofundishwa leo, lakini lazima tujue kwamba, kama wafuasi wa Kristo, tunatakiwa kujikana, kubeba msalaba wetu, na kumfuata Yesu.

Mtume Paulo anatuambia katika Warumi 12 kwamba hatutakiwi kufanana na ulimwengu huu, bali tugeuzwe kwa kufanywa upya nia zetu, tupate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu. Neno hili, kufanywa upya, linatokana na neno la kiyunani, anakainosis, ambalo maana yake ni kukarabati. Katika muktadha huu, ina maana tunatakiwa kuachana na njia zetu za zamani za kidunia za kufikiri, kutenda, na kuishi, na kuanza kuzibadilisha na vitu vya Mungu.

Katika 1 Yohana 2:15-20, inatupa tahadhali kuhusu wale wanaopenda dunia, itakachofanya, na inamaanisha nini hasa. Inasema kama mtu akiipenda dunia, upendo wa Baba hauko ndani yake. Pia inazugumza juu ya kitambo kidogo cha tamaa za dunia na mambo yake yote. Lakini wote wafanyao mapenzi ya Mungu huishi milele.

Tunapoanza mpango huu wa siku 21, lazima tujitahidi kuachana na upendo wa dunia. Hatuwezi kutumikia mabwana wawili - lazima tumchague Mungu au dunia. Tutakapomchagua Mungu, lazima tuachane na upendo usio wa Mungu na ambao bado unakaa mioyoni mwetu.

Kuhusu Mpango huu

21 Days to Overflow

Katika siku 21 za kufurika mpango wa YouVersion, Jeremiah Hosford atawachukua wasomaji safari ya majuma 3 ya kujimimina wao kwa wao, kujawa na Roho Mtakatifu, na kuacha mafuriko, na maisha yaliyojaa Roho. Ni wakati wa kuacha kuishi kawaida na kuanza kuishi maisha ya kufurika!

More

Tungependa Kuishukuru YouVersion kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya https://www.theartofleadership.com/