Siku 21 za KufurikaMfano

Kupata Uzoefu wa Udhihirishoi wa Uwepo wa Mungu
Tunapohitimisha juma la pili la mpango huu, hebu tuangalie kupata uzoefu wa udhihirisho wa uwepo wa Mungu.
Tunapotaka uwepo wa Mungu kuliko kitu kingine chochote, kuliko nyumba mpya, kupanda cheo, au gari jipya, Ataonekana katika sehemu zote tunazomtafuta.
Tumeitwa ili kuzoea uwepo wa Mungu. Hii imekuwa ni tabia iliyopotea katika kanisa la leo. Wengi hawajui hata namna ya kuzoea udhihirisho wa uwepo wa Mungu, kwa sababu hawana hata wazo kuwa hicho ni nini. Katika mipango ya ibada zetu za jumla, tumetawaliwa sana na kuingia na kutoka kwa muda fulani ambao hatuachi hata nafasi kwa ajili ya Mungu kudhihirisha uwepo wake katikati yetu. Mungu haji katika mipango yetu.
Hebu turudi nyuma kwenye Yohana 14:21. Katika mstari huu, Yesu anasema yeye ampendaye atapendwa na Baba na Yeye (Yesu) atajidhihirisha kwao!
Katika Kutoka 33:1-3 na 12-16, Mungu anampa Musa maagizo kwa ajili ya kuwaongoza wana wa Israeli. Wakati Musa alipojisikia kwamba hawezi kukabiliana na changamoto alimuomba Mungu, Mungu anamwambia atatuma uwepo wake kuwaongoza. Wakati uwepo wa Mungu katika agano la kale ilikuwa ni nguzo ya wingu mchana na nguzo ya moto usiku, sasa hivi anajifunua tofauti. Kupitia sadaka ya Kristo ns Roho Mtakatifu kukaa ndani yetu, sasa anaweza kujifunua kupitia kwetu.
Kwa shauku sana tunahitaji udhihirisho wa uwepo wa Mungu. Kama vyote tulivyo navyo ni ahadi, tumekosa jambo la muhimu sana. Tusikubali kuishi siku moja bila udhihirisho wa uwepo wa Mungu. Tusiridhike na ibada za kanisa, mikutano ya maombi, au huduma zozote zile bila udhihirisho wa uwepo wa Mungu. Ni uwepo wake utakaoleta tofauti. Yesu alisema kama tukimpenda na kushika amri zake, atajidhihirisha kwetu. Tuliumbwa kwa ajili yake.
Kuhusu Mpango huu

Katika siku 21 za kufurika mpango wa YouVersion, Jeremiah Hosford atawachukua wasomaji safari ya majuma 3 ya kujimimina wao kwa wao, kujawa na Roho Mtakatifu, na kuacha mafuriko, na maisha yaliyojaa Roho. Ni wakati wa kuacha kuishi kawaida na kuanza kuishi maisha ya kufurika!
More