Siku 21 za KufurikaMfano

Upako wa Roho Mtakatifu
. Tulianza kwa kuondoa kila kitu kilichokuwa kikichafua maisha yetu na safari yetu na Mungu. Kisha tukajaza hizo nafasi tupu na Utu na Uwepo wa Roho Mtakatifu. Sasa tunajifunza kuishi katika mtindo wa maisha unaofurikwa na Roho Mtakatifu. Hii ilianza kwa kumgundua au kugundua upya kwamba Roho Mtakatifu anataka ushirika na sisi mara kwa mara. Leo tutaingia ndani zaidi.
Mara nyingi kwenye Agano la Kale, maji huwakilisha uwepo na kazi ya Roho Mtakatifu. Tunapotumia ishara ya unabii huu katika maisha yetu, tunaona kuna viwango tofauti vya upako wa Roho Mtakatifu tunavyoweza kuchagua kufanyia kazi. Kwa baadhi yetu tunafanya kazi kwenye upako wenye kina kinachofikia kufundo cha mguu. Baadhi yetu tupo kiuoni, wengine shingoni. Lakini kuna mikondo mikali kwenye mto wa Mungu inayotuweka kwenye nafasi ambayo hatuhitaji kusimama wenyewe bali tunatembea kwenye mtiririko wa Mungu.
Kwenye 1 Yoh 2:27 tunaona inarejea upako wa Roho Mtakatifu. Tunaona tena kwenye Isaya 10:27 inarejea kwenye upako, katikati ya unabii wa mabaki ya Israeli. Kwenye kifungu hiki tunaona upako wa Roho Mtakatifu una nguvu kubwa, kama mstari unavyosema, ''unaweza kuharibu nira" na mzigo. Lazima tukiri mbele ya Mungu hamu yetu ya kutoka kwenye kina cha kifundo cha mguu na cha kiuno tunachofanyia kazi. Tunahitaji kumuomba Mungu ongezeko litakalokuwezesha kuogelea - ili kupata upako kamili wa Roho Mtakatifu.Andiko
Kuhusu Mpango huu

Katika siku 21 za kufurika mpango wa YouVersion, Jeremiah Hosford atawachukua wasomaji safari ya majuma 3 ya kujimimina wao kwa wao, kujawa na Roho Mtakatifu, na kuacha mafuriko, na maisha yaliyojaa Roho. Ni wakati wa kuacha kuishi kawaida na kuanza kuishi maisha ya kufurika!
More