Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Siku 21 za KufurikaMfano

21 Days to Overflow

SIKU 18 YA 21

Ndoto na Maono

Tunawezaje kuitambua sauti ya Mungu? Kwanza kabisa, huzungumza kupitia neno lake, Biblia. Kila anapozungumza kwa njia zingine, mara zote kutaendana na neno lake.

Huzungumza nasi katika maombi.

Huzungumza nasi kupitia waamini wengine, viongozi wetu, na manabii.

Huzungumza kupitia ndoto na maono.

Katika Yoeli 2:28-29, kati kati ya unabii wake kuhusiana na Siku ya Bwana, aliandika juu ya kumimiminwa kwa Roho Mtakatifu katika siku za mwisho. Inasema kwamba "wana wenu wa kike na wa kiume watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono."

Tunaweza tusijue siku za mwisho zitatokea wakati gani, lakini kujua juu ya unabii huu, lazima tuwe tayari kushuhudia hizi ndoto na maono--na kuzisikiliza zinapotokea.

Katika Hesabu 12:6, tunaona Bwana akithibitisha ukweli wa ndoto na maono za manabii anaowatuma.

Tunapopata ndoto au kuona maono, kitu cha kwanza tunachotakiwa kufanya ni kumuuliza Mungu, " Hii inatoka kwako?" Tunapothibitisha kupitia neno lake na kudhihirika kwa uwepo wake utokao kwake, lazima tuulize tena, "Natakiwa kufanya nini?" Alitoa kwa kusudi, kwa hiyo lazima tufafute kusudi lake.

Ninaamini tunaishi katika siku za mwisho, na Mungu ameahidi kwamba atazungumza nasi katika ndoto na maono katika siku za mwisho. Lazima tumtarajie kuzungumza nasi kwa njia hii na kusikiliza kwa makini afanyapo hivyo.

Kuhusu Mpango huu

21 Days to Overflow

Katika siku 21 za kufurika mpango wa YouVersion, Jeremiah Hosford atawachukua wasomaji safari ya majuma 3 ya kujimimina wao kwa wao, kujawa na Roho Mtakatifu, na kuacha mafuriko, na maisha yaliyojaa Roho. Ni wakati wa kuacha kuishi kawaida na kuanza kuishi maisha ya kufurika!

More

Tungependa Kuishukuru YouVersion kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya https://www.theartofleadership.com/