Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Siku 21 za KufurikaMfano

21 Days to Overflow

SIKU 19 YA 21

Kuona Kama Mungu Anavyoona

Mara nyingi, tunadhani hakuna kinachotokea kama hatuwezi kukiona, lakini sivyo ilivyo. Hebu fikiria hivi. Kama kuna kazi inafanyika nje ya eneo ulilopo, na huwezi kuiona, ina maanisha kazi hiyo haifanyiki, kwa sababu ya wewe kukosa uwezo wa kuiona? Au kama huwezi kuona ndani ya duka lililopo ng'ambo ya nyumba yako, ina maanisha hakuna wanunuzi? Hakika sivyo. Hata hivyo, hivi ndivyo wengi tunavyochagua kuishi maisha yetu. Tumeokoka, tumejazwa na Roho, na waaminifu kwa Mungu na kanisa lake, lakini tunatambua kwamba Shetani siku zote anafanya kazi katika ulimwengu wake, na ndivyo ilivyo kwa majeshi ya mbinguni.

Macho ya ufahamu wetu yatiwe nuru, ili tujue tumaini la wito wake. Kwa njia hiyo hatuwi na ufahamu wa juu juu au maarifa ya wito wake. Badala yake tunaweza kujua kina cha wito wake. Tunaweza kujua anataka tufanye nini na wito wetu.

Katika Waefeso 1:17-21, inazungumza juu ya kutiwa nuru. Paulo anasema katika maombi yake kwamba " macho ya mioyo yenu yatiwe nuru mjue tumaini la wito wake".

Baadaye katika Waefeso 6:12-17, Paulo anazungumza kuhusu silaha za Mungu. Silaha hizi --pamoja na utofauti wake -- zinatokana na ufahamu mzuri wa Mungu, kweli yake, wokovu, na kupokea haki ya Yesu --dirii ya haki. Silaha hizi zinatuwezesha "kuizima" mishale yote ya moto ya adui.

Lakini hatutakiwi kujilinda peke yake! Upanga wetu, ambao Paulo anauita "upanga wa roho," unaturuhusu kusimama dhidi ya adui.

Mtiririko huu ambao umekuwa unaupata umetengeneza njia tuu. Wakati macho yako ya ufahamu yanapotiwa nuru, utatembea katika uwepo wa Mungu ambao haujawahi ona. Mungu anaweza na anatamani kufungua ulimwengu ambao haufungwi na muda, eneo la kijiografia, au uwezo wa mwanadamu.

Kuhusu Mpango huu

21 Days to Overflow

Katika siku 21 za kufurika mpango wa YouVersion, Jeremiah Hosford atawachukua wasomaji safari ya majuma 3 ya kujimimina wao kwa wao, kujawa na Roho Mtakatifu, na kuacha mafuriko, na maisha yaliyojaa Roho. Ni wakati wa kuacha kuishi kawaida na kuanza kuishi maisha ya kufurika!

More

Tungependa Kuishukuru YouVersion kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya https://www.theartofleadership.com/