Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Siku 21 za KufurikaMfano

21 Days to Overflow

SIKU 17 YA 21

Moto Mpya

Pasipokujali dhehebu, ubatizo wa Roho Mtakatifu upo kwa kila mwamini.

Na, zaidi, ubatizo katika Roho Mtakatifu ni kwa ajili yako sasa hivi. Anakutaka ujazwe na moto wake. Anataka utiwe nguvu kwa uwepo wake ukitenda kazi ndani yako na kupitia kwako.

Unaamini anataka kukujaza na Roho wake? Una amini anataka kukujaza na moto mpya?

Katika Matendo ya Mitume 2:1-4, tunaona Roho Mtakatifu akijidhihirisha kupitia mwili wa kanisa walipoanza kunena kwa lugha.

Katika Matendo ya Mitume 4:1-8, tunamuona Petro, akiwa na Yohana, walilala gerezani hata asubuhi na kuhojiwa mbele ya Anasi, Kuhani Mkuu, na wale waliokuwa jamaa zake. Walipokabiliwa na hali hii ya kuogofya, inasema Petro alijawa na Roho Mtakatifu!

Ingekuwaje kama Mungu alitaka kutujaza na Roho Mtakatifu katika ya nyakati zetu ngumu, lakini hatuko wazi kwa hilo? Nini kinatakiwa kubadilika katika maisha yako na moyo wako kufungua mlango kwa ajili ya moto mpya wa Roho Mtakatifu?

Katika Mathayo 3:11-17, mwanzo kabla ya kueleza habari za ubatizo wa Yesu na Yohana Mbatizaji, Yohana anazungumza juu ya ubatizo wa nguvu. Siyo wa maji, bali wa moto. Siyo kwa mkono wake, bali wa Roho Mtakatifu.

Imani ileile iliyokuchukua ili kuzaliwa mara ya pili ni imani ileile itakuchukua ili kujazwa na Roho Mtakatifu. Bwana anataka kukubatiza katika Roho Mtakatifu na moto!

Kuhusu Mpango huu

21 Days to Overflow

Katika siku 21 za kufurika mpango wa YouVersion, Jeremiah Hosford atawachukua wasomaji safari ya majuma 3 ya kujimimina wao kwa wao, kujawa na Roho Mtakatifu, na kuacha mafuriko, na maisha yaliyojaa Roho. Ni wakati wa kuacha kuishi kawaida na kuanza kuishi maisha ya kufurika!

More

Tungependa Kuishukuru YouVersion kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya https://www.theartofleadership.com/