Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kuhusu YouVersion

Umuhimu

Katika kipindi cha vizazi vilivyopita, watu kupata Biblia ilikuwa nadra mno. Leo, hii kesi imebadilika. Hata hivyo, watu wengi ambao wanapata Biblia wanafikiri ujumbe wake hauwahusu maishani mwao. Wakati huo huo, kuna wengine ambao wanaamini kuwa kuna uhusiano kati ya Biblia na uzoefu wao kila siku.

Mapinduzi ya habari

Katika muongo uliopita, Internet imeleta mapinduzi yanayotia watu nguvu amabayo hijaonekana mbeleni. Pamoja na uwezo wa kushiriki, kuchangia, kujenga, kutangaza na kuwasiliana, ni rahisi kueleza sisi ni nani na nini tunaamini pamoja na dunia nzima.

YouVersion

Tangu ilipoanza mwaka wa 1996, Kusudi la Life.Church limekuwa kuwaongoza watu wawe wafuasi waliojitoa kikamilifu wa Kristo. Kwa kufanya hivyo, tumetafuta njia mpya za kuwasaidia watu kuunganisha Biblia na maisha yao ya kila siku. Mbinu zetu zimebadilika kwa miaka mingi kwani tumejumuisha teknolojia na mikakati mbalimbali. Lakini kimsingi, mtazamo wetu unabaki kwenye umuhimu tunapojitahidi mara kwa mara kuwaonyesha na kuwafundisha watu jinsi Neno la Mungu linavyohusiana na kila mtu, haijalishi yuko wapi maishani. YouVersion inawakilisha mpaka mpya katika juhudi za Life.Church. Hatutengenezi tu zana ya kuathiri ulimwengu kwa kutumia teknolojia ya kibunifu, muhimu zaidi, tunashirikisha watu katika uhusiano na Mungu wanapogundua umuhimu wa Biblia kwenye maisha yao.

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha