Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Siku 21 za KufurikaMfano

21 Days to Overflow

SIKU 20 YA 21

Imani Na Matendo

Kufurika kunafanya kazi na imani isivyo ya kawaida. Ina fanya kilichokuwa hakiwezekani kuwezekana. Hiki ndicho kinatokea tunapokuwa na imani katika Mungu na kutembea katika hali isiyokuwa ya kawaida.

Kama hatuna imani, hatuwezi kumpendeza Mungu. Uhusiano wetu na Mungu unategemea imani. Tunapozaliwa mara ya pili, hakuna awezaye kuthibitisha wokovu wetu kwa kitu wanachoweza kutupa. Hata kama wangetupa cheti ambacho kinasema tumeokoka, hakina maana yoyote. Wokovu wetu unathibitishwa na imani tuliyoiweka kwa Bwana Yesu Kristo kusamehe dhambi zetu na kututakasa na udhalimu wote. Kama tulivyoonesha imani kwa kuzaliwa mara ya pili, tunaendelea kumuishia Mungu kwa imani. Inahitaji imani kuwa na uhusiano wa kila siku na Yesu Kristo. Inahitaji imani kuomba, kushuhudia, kutoa, na kutumika. Kila kitu kuhusu uhusiano wetu na Mungu unasimama katika imani. Ndiyo maana haiwezekani kumpendeza Mungu pasipo imani.

Huniamini kwamba haiwezekani kumpendeza Mungu pasipo imani? Hebu angalia katika Waebrania 11:6. Imani yetu ni kiungo muhimu kumpendeza Mungu!

Waebrania 11 yote ni sura ya ajabu sana ambayo inajadili kuhusu imani kupitia neno la Mungu na maana halisi ya imani. Kutoka Nuhu mpaka imani ya Ibrahimu mpaka Musa na Yakobo, inagawanya hadithi za Biblia na jinsi zilivyoonyesha imani katika Bwana.

Na habari njema ni kwamba, wote tunayo imani! Warumi 12:3 inazungumza juu ya hilo. Kila mmoja anatakiwa kujitahidi kuizoeza hii imani katika Mungu na kumwamini kwa kila anachofanya.

Karibu kila wakati Yesu alipowakemea wanafunzi wake, ilikuwa ni kwa kukosa imani. Hivi ndivyo Mungu anavyoitazama imani. Kukosa imani kunakaribisha karipio kutoka kwake. Hii ndiyo sababu majaribu huja katika maisha yetu. Hii ndiyo sababu Mungu anaruhusu mambo yatokee katika maisha yetu ambayo yeye tuu anaweza kuyatatua. Yote haya yanaongeza imani yetu. Tunatakiwa kuishi kwa imani na kila siku kukua. Haya huruhusu nguvu isiyo yakawaida ya Mungu kujidhihirisha ndani yetu.

Mashambulizi mengi unayokabiliana nayo yana uhusiano mdogo sana na kile unachokabiliana nacho. Yana uhusiano mdogo sana na wewe jinsi ulivyo. Yanahusiana sana na vile unavyotakiwa kuwa. Kwa hiyo, Shetani anakushambulia sasa, ili aweze kushambulia kesho yako. Ni vita dhidi ya imani yako, kukuondoa katika hatima yako. Kama tutaruhusu imani yetu kuchochewa na kujengwa, tunaweza kuzima mashambulizi na kujihakikishia hatima yetu.

Kuhusu Mpango huu

21 Days to Overflow

Katika siku 21 za kufurika mpango wa YouVersion, Jeremiah Hosford atawachukua wasomaji safari ya majuma 3 ya kujimimina wao kwa wao, kujawa na Roho Mtakatifu, na kuacha mafuriko, na maisha yaliyojaa Roho. Ni wakati wa kuacha kuishi kawaida na kuanza kuishi maisha ya kufurika!

More

Tungependa Kuishukuru YouVersion kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya https://www.theartofleadership.com/