Siku 21 za KufurikaMfano

Kumkaribia Mungu
Kumkaribia Mungu maana yake ni kumtafuta Mungu kwa mioyo yetu yote. Kiki ndiyo kufunga na kuomba humaanisha. Hatuko katika mgomo wa kula kumlazimisha Mungu afanye kitu. Badala yake, tunajinyenyekeza kupitia kufunga na kuomba ili Mungu atubadilishe na kutuweka ili kutembea katika mapenzi yake. Tunaondoa vizuizi vinavyozuia maombi yetu ili yasifike masikioni mwa Mungu. Ni kuhusu kumtafuta Mungu kwa kila tulichonacho.
Tumesoma kifungu cha Yakobo 4:1-10 hapo mwanzo kwenye mpango huu, lakini ngoja tukiangalie tena. Kinazungumza juu ya kiburi na utii. Kinatutaka kuwa watii kwa Mungu ili kumkaribia na mambo yote mazuri yatokanayo na uamuzi huu wa kutii.
Katika 2 Mambo ya Nyakati 15:1-2, tunaona Roho wa Mungu akiwasiliana na Azaria, mwana wa Obedi. Azaria anamwambia Asa kwamba kama atamtafuta Mungu na mambo yake, Mungu atakuwa pamoja naye. Lakini kama Azaria atamuacha Mungu na hatamkaribia, Mungu atamuacha.
Wakati mioyo yetu inapochafuliwa, tunatengeneza ugumu kwa mambo ya Mungu. Wakati mioyo yetu inapokuwa migumu kwa mambo ya Mungu, hatuwezi kumkaribia Mungu. Kumkaribia Mungu, lazima nijitakase (kujimimina), kutii kweli kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu, na kwa bidii na upendo wa kweli na moyo safi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Katika siku 21 za kufurika mpango wa YouVersion, Jeremiah Hosford atawachukua wasomaji safari ya majuma 3 ya kujimimina wao kwa wao, kujawa na Roho Mtakatifu, na kuacha mafuriko, na maisha yaliyojaa Roho. Ni wakati wa kuacha kuishi kawaida na kuanza kuishi maisha ya kufurika!
More