Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Siku 21 za KufurikaMfano

21 Days to Overflow

SIKU 12 YA 21

Kukaa katika Upendo wa Mungu

Jana, tulimuomba Mungu atuongezee upendo kwake na kwa wengine. Leo, tutaenda kujifunza jinsi ya kukaa katika huu upendo ulioongezwa.

Kukaa maana yake kuishi ndani yake, au kukaa ndani, kwa namna hiyo hiyo tunaishi ndani, au kukaa ndani ya nyumba yetu. Ni mahali tunakaa. Kukaa katika upendo maana yake ni kwamba tunaweza kukutwa tunakaa katika upendo. Tunapotakiwa kukutwa, tunaweza kukutwa katika upendo, kama tutakaa katika upendo. Masomo yetu kutoka Injili ya Yohana sura ya kumi na tano inatuonesha kweli nyingi zenye nguvu juu ya kukaa katika upendo inavyoonekana.

Yohana 15:7-9 Inazungumza kuhusu nguvu ya kukaa katika upendo wa Mungu. Inasema tunapokaa ndani yake na neno lake kukaa ndani yetu, tunaweza kuomba lolote nasi tutapewa. Anafanya hivyo kwa utukufu wake! Anapenda kuona watoto wake wakifanikiwa kama agano la nguvu zake, neema yake, na rehema zake.

Katika Yohana 15:26, inazungumza habari ya Roho Mtakatifu. Kupitia mapungufu yetu na madhaifu yetu, Roho Mtakatifu anashuhudia juu ya wema wa Mungu. Kupitia ukamilifu wa Mungu kwetu na kukubali kutokukamilika kwetu, tunamletea yeye utukufu.

Tunapokaa katika upendo wake, Roho Mtakatifu huja na kuambatana nasi, hutujaza na kufurika. Kabla hatutajua, upendo wa Mungu hufanya kazi ndani yetu kwa namna ambayo mambo yaliyozoea kutuangusha, kutuweka macho, kuturudisha nyuma, na kutufanya tuchukie, hayawezi tena kutufanya vitu hivyo. Tunakuwa hatushindikani tunapokaa kwenye upendo.

Kuhusu Mpango huu

21 Days to Overflow

Katika siku 21 za kufurika mpango wa YouVersion, Jeremiah Hosford atawachukua wasomaji safari ya majuma 3 ya kujimimina wao kwa wao, kujawa na Roho Mtakatifu, na kuacha mafuriko, na maisha yaliyojaa Roho. Ni wakati wa kuacha kuishi kawaida na kuanza kuishi maisha ya kufurika!

More

Tungependa Kuishukuru YouVersion kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya https://www.theartofleadership.com/