Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Siku 21 za KufurikaMfano

21 Days to Overflow

SIKU 7 YA 21

Kutokusamehe

Kutokusamehe ni uovu. Ni uharibifu kiroho, kihisia, na kimwili pia. Kunachukua na kuchukua, pasipo kurejesha. Kuna zaidi, tunaona katika maandiko kwamba msamaha wetu kutoka kwa Mungu ni kutokana na kuwasamehe wengine. Umilele, yaani mbinguni na jehanamu kunategemea utayari wetu kusamehe. Hatma ya nafsi zetu inategemea uamuzi wetu wa kusamehe, au kutokusameheana.

Mathayo 6:14-15 inaweka kanuni hii wazi kabisa. Tunapowasamehe ndugu zetu na dada zetu waliotukosea, Mungu atatusamehe. Lakini tusipoonesha msamaha, Mungu hatatusamehe.

Waefeso 4:32 inaendelea kusema tunahitaji kuonesha msamaha ambao Kristo Mungu ametuonesha kwanza. Tunahitaji kuonesha huruma kwa ndugu na dada zetu. Yawezekanaje kutokusamehe? Hatukustahili msamaha wa Mungu aliotuonesha. Yawezekanaje kusema mtu fulani hastahili msamaha wetu?

Elewa hili: hatuwasamehi watu kwa ajili yao. Tunawasamehe kwa ajili yetu wenyewe. Kutomsamehe mtu haimaanishi kuwa wako kifungoni. Kuna uhuru unaokuja tunaposamehe. Tunapoomba leo, minyororo inayovunjika itakuwa inavunjika kutoka kwetu. Hata kama watu hawatusamehi, haijalishi. Tutakuwa huru. Tutapatanishwa na Mungu.

Kuhusu Mpango huu

21 Days to Overflow

Katika siku 21 za kufurika mpango wa YouVersion, Jeremiah Hosford atawachukua wasomaji safari ya majuma 3 ya kujimimina wao kwa wao, kujawa na Roho Mtakatifu, na kuacha mafuriko, na maisha yaliyojaa Roho. Ni wakati wa kuacha kuishi kawaida na kuanza kuishi maisha ya kufurika!

More

Tungependa Kuishukuru YouVersion kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya https://www.theartofleadership.com/