Siku 21 za KufurikaMfano

Ubinafsi
Leo, tunaangalia jinsi ya kuachana na kitu ambacho kimekuwa cha kawaida sana katika ulimwengu wa leo: ubinafsi.
Tunachofanya, siyo tuu kanisani, lakini nje ya kanisa hakiwezi kufanyika kwa nia ya roho ya ubinafsi na kificho. Ikiwa tuko kazini, shuleni, na marafiki, na familia, sokoni, au tunatumika kama viongozi, nia zetu ni muhimu sana.
Swali ambalo tunatakiwa kujiuliza siyo,"Kipi bora kwangu?" Badala yake, tunatakiwa kujiuliza, " Ni kipi bora kwa ajili ya ufalme wa Mungu?" Tamaa yetu inatakiwa kuwa ni kutafuta njia bora ya kufanya mapenzi kamili ya Mungu.
Katika Wafilipi 2:3-4 inasema msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno. Hakuna kinachomaanisha chochote. Tunapofanya kila kitu kwa ajili ya ufalme wa Mungu badala yetu wenyewe, ni jinsi gani maisha yetu yataonekana tofauti?
1 Wakorintho 10:24 inaangazia kanuni hii, mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya wenzake. Ni jinsi gani kanisa lingekuwa leo kama kila mtu angekuwa anafanya kwa faida za wenzake? Ni jinsi gani ulimwengu ungekuwa kama kusingekuwa na mtu anayefanya kwa tamaa yake bali kwa faida ya wengine?
Siku nyingine tunapojaribu kufanya kitu kwa ajili ya wengine, au kwa ajili ya Bwana, tumuombe Bwana atufunulie kama nia zetu ni za kibinafsi. /p>
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Katika siku 21 za kufurika mpango wa YouVersion, Jeremiah Hosford atawachukua wasomaji safari ya majuma 3 ya kujimimina wao kwa wao, kujawa na Roho Mtakatifu, na kuacha mafuriko, na maisha yaliyojaa Roho. Ni wakati wa kuacha kuishi kawaida na kuanza kuishi maisha ya kufurika!
More