Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Siku 21 za KufurikaMfano

21 Days to Overflow

SIKU 3 YA 21

Udanganyifu

Kitu kinachofuata ambacho inabidi tukiondoe ili tuishi maisha yaliyojaa Roho, maisha yaliyofurika ni udanganyifu wa adui.

Katika Yohana 8:44, inamwita shetani mwongo. Lakini si mwongo tuu -inamuita baba wa uongo. Hiki ndiyo cheo na hakitolewi kwa mwongo wa kawaida. Adui yetu ni bwana wa udanganyifu. Kwa kutambua hilo yatupasa kuingia kwenye mapambano ya kujilinda na udanyanyifu wowote anaouleta duniani.

Katika Wagalatia 6:7-8, Paulo analiambia kanisa la Galatia wasidanganyike. Hata wakati ule, na hasa sasa, adui yuko kazini akipotosha neno la Mungu, akiwachanganya watoto wake, na kufifisha maadili. Hatuwe kujiacha kuwa wahanga wa udanganyifu wake.

Badala yake, tunahitaji kujikita katika kweli ya neno la Mungu. Tukifanya hivyo, tunajiepusha na udanganyifu wa adui na tunaweza kuendelea kutembea katika mapenzi ya Mungu pasipo kuyumba.

Kuhusu Mpango huu

21 Days to Overflow

Katika siku 21 za kufurika mpango wa YouVersion, Jeremiah Hosford atawachukua wasomaji safari ya majuma 3 ya kujimimina wao kwa wao, kujawa na Roho Mtakatifu, na kuacha mafuriko, na maisha yaliyojaa Roho. Ni wakati wa kuacha kuishi kawaida na kuanza kuishi maisha ya kufurika!

More

Tungependa Kuishukuru YouVersion kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya https://www.theartofleadership.com/