Siku 21 za KufurikaMfano

Kiburi
Tumefikia siku ya tano ya kujimimina wenyewe. Hii haijawa rahisi!
Ni mara ngapi Mungu ametutaka kufanya jambo, na ama hatujalifanya, au tumelifanya nusu? Hiki ni kiburi. Hapo ni sisi tunasema, " Mimi ni Mungu, na ninajua kilichobora kwangu katika mazingira haya."
Kiburi kinatawala katika ulimwengu wa sasa. Kiburi ni majivuno binafsi, kiburi cha kipato, kiburi cha uwezo, kiburi cha familia, na zaidi. Kiburi hiki kinatuweka mbali na Mungu na kutufanya tujiangalie wenyewe na kile tunachoweza kukifanya.
Katika Yakobo 4:6-8, Yakobo anasema Mungu huwapinga wajikuzao bali huwapa neema wanyenyekevu. Tunahitaji kujinyenyekeza machoni pa Bwana ili tupate neema yake. Tunapotambua tulivyo na vile tulivyofanya ni baraka kutoka kwa Bwana, hatuna sababu ya kuwa na kiburi.
Mithali 16:18 inaongeza hatari ya kiburi kwa kusema hutangulia uangamivu. Kiburi hutangulia uangamivu! Kama tunajua hilo ni kweli, kwa nini tunaendelea kuweka kiburi kwa mambo madogo maishani mwetu?
Kuishi maisha yalliyojaa, lazima tukiondoe kiburi. Tukitaka kujawa na Roho, hakuna nafasi ya kiburi. Omba na umuombe Bwana akufunulie kiburi chochote kilichojificha katika maisha yako ili uweze kumfuata kikamilifu.
Kuhusu Mpango huu

Katika siku 21 za kufurika mpango wa YouVersion, Jeremiah Hosford atawachukua wasomaji safari ya majuma 3 ya kujimimina wao kwa wao, kujawa na Roho Mtakatifu, na kuacha mafuriko, na maisha yaliyojaa Roho. Ni wakati wa kuacha kuishi kawaida na kuanza kuishi maisha ya kufurika!
More