Siku 21 za KufurikaMfano

Kiu ya Kiroho
Umetenda! Ulivumilia maumivu na kazi ngumu ya kujimimina ambavyo vingeweza kukuzuia kupokea yote Mungu aliyonayo kwa ajili yako. Kwa siku saba zilizopita, umejinyenyekeza, umejichunguza, na kuondoa vitu vyote vinavyotosheleza mwili wako. Haikuwa rahisi, lakini imestahili.
Kwa siku saba zifuatazo, tunaelekeza mioyo yetu katika kujazwa na Roho Mtakatifu. Nafasi tulizozitengeneza katika maisha yetu sasa zinakaribia kujazwa na ujazo wa Mungu. Kuna mabadiliko yasiyo mithilika yakija katika maisha. Jiweke tayari kwa mabadiliko ya maisha.
Katika Yohana 4:13-14, inaeleza juu ya kiu ya kiroho. Mambo ya dunia hii-maji ambayo Yesu anayataja- yatakata kiu kwa muda tuu, lakini utapata kiu tena. Ndipo anaendelea kuzungumza juu ya maji ambayo hutaona kiu tena. Maji haya ni Roho Mtakatifu. Haya yanatakiwa kuwa maji tunayoyataka.
Katika Yohana 7:37-39, Yesu anaendelea anaposema, " mtu akiona kiu na aje kwangu anywe." Kumpokea Roho Mtakatifu, maji haya ya milele, tunahitaji kumpokea Yesu na kuamini kile alichotuambia katika neno la Mungu.
Hatutakiwi kwenda tuu kwa mkumbo. Tunatakiwa kuona kiu ya maji yaliyo hai ambayo ni Roho Mtakatifu tuu anaweza kutupa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Katika siku 21 za kufurika mpango wa YouVersion, Jeremiah Hosford atawachukua wasomaji safari ya majuma 3 ya kujimimina wao kwa wao, kujawa na Roho Mtakatifu, na kuacha mafuriko, na maisha yaliyojaa Roho. Ni wakati wa kuacha kuishi kawaida na kuanza kuishi maisha ya kufurika!
More