Siku 21 za KufurikaMfano

Vikekengeushi
Leo, tunaangalia kuondoa vikengeushi ambavyo dunia hii inatuletea kwa wingi. Hatuwezi kumfuata Mungu kikamilifu na mapenzi yake kwa ajili ya maisha yetu na kuwa, na maisha yaliyojaa kiroho kama mara kwa mara tunakengeuka.
Katika Wafilipi 4:8, Paulo anatoa maagizo kwa kanisa la Filipi kuhusu wanachotakiwa kukitafakari. Japo kifungu hiki kinaeleza kile tuu ambacho alitaka kanisa kutafakari, kinaweza kikaashiria kile ambacho hakukisema. Msongo, wasiwasi na hofu havimo katika orodha ya Paulo kwa kanisa la Filipi. Badala yake, aliwaambia watafakari yaliyo ya kweli, yaliyo ya staha, yaliyo safi, yaliyo ya kupendeza, yoyote yenye sifa njema na haki.Tunapochukua hatua hii, tunakuwa hatua moja karibu na kutafakari kama Mungu anavyotamani na kujilinda na ukengeufu.
Katika Yohana 17:17, tunaona Yesu akiwaombea wanafunzi wake. Anamuomba Mungu awatakase na kweli yake. Ni nini anachoendelea kukiita kweli ya Mungu? Neno lake. Hii inatupa ufahamu juu ya kile Paulo alichokuwa anakisema wakati alipowaambia kanisa la Filipi kutafakari yoyote yaliyo ya kweli.
Tunatakiwa kukaa katika kweli ya Neno la Mungu. Hili linapokuwa na umuhimu katika maisha yetu, hatutaweza kukengeushwa kirahisi na mambo ya dunia hii. Hii ni hatua ya maana katika kuishi maisha yaliyojawa na Roho, maisha ya kufurika.
Kuhusu Mpango huu

Katika siku 21 za kufurika mpango wa YouVersion, Jeremiah Hosford atawachukua wasomaji safari ya majuma 3 ya kujimimina wao kwa wao, kujawa na Roho Mtakatifu, na kuacha mafuriko, na maisha yaliyojaa Roho. Ni wakati wa kuacha kuishi kawaida na kuanza kuishi maisha ya kufurika!
More