Siku 21 za KufurikaMfano

Kosa
Umewaki kukosewa?
Kosa ni moja ya silaha muhimu ambazo Shetani anatumia katika kampeni yake kuwazuia watu wa Mungu. Anawaangusha hata watu wenye nguvu. Anatumia makosa kuufanya ufalme wa Mungu kutokuwa na nguvu. Anatumia makosa kuharibu makanisa. Anatumia makosa kuharibu familia. Anatumia makosa kugawanya washarika. Anatumia makosa kuharibu hisia, akili, na hata magonjwa ya mwili kwa watu.
Mithali 17:9 inasema afunikaye makosa hutafuta kupendwa, bali yeye akashifuye neno, hutenga rafiki. Kufuta kosa haimaniishi hulikumbuki na umesahau moja kwa moja. Haimaanishi hulikumbuki na wala huna kinyongo na kaka au dada yako. Ina maana umevuka hatua hiyo na kuonesha msamaha Mungu aliokuonesha kwa wanaokuzunguka.
Katika Waebrania 12:15, inasema mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu. Neema hii, ilioneshwa kwetu na Mungu kwa ajili ya dhambi zetu, lazima uendelee mbele. Lazima tuwe na haraka kusamehe waliotukosea! Kiini cha uchungu ambao hupelekea matatizo. Chanzo hiki kinaweza kuainishwa kwa njia nyingi, lakini kwa ufupi, ni kosa. Hatuwezi kuwaacha watu watukosee kiasi cha kuweka uchungu juu yao mioyoni mwetu.
Tusiache kosa likakaa katika maisha yetu. Usamehe haraka na haraka kuomba msamaha kwa wengine. Tukitaka kujawa na kufurika katika Roho, hatuwezi kuacha kosa likawa kichocheo katika maisha yetu!
Kuhusu Mpango huu

Katika siku 21 za kufurika mpango wa YouVersion, Jeremiah Hosford atawachukua wasomaji safari ya majuma 3 ya kujimimina wao kwa wao, kujawa na Roho Mtakatifu, na kuacha mafuriko, na maisha yaliyojaa Roho. Ni wakati wa kuacha kuishi kawaida na kuanza kuishi maisha ya kufurika!
More