Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

SIKU 1 YA 28

Ni haki kabisa kumwita Abramu baba wa imani. Leo twaona imani yake kwa Mungu. 1.Mtu kuhama halikuwa jambo la kawaida wakati ule. Tena mtu kuachana na baba yake na ukoo wake na kuhamia nchi iliyokuwa mbali ni tendo la ajabu sana (m.1,Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako).2.Hakujua mahali aendako, nchi ya Kanaani kwake ni ugenini kabisa. Alijua tu kwamba Mungu atamwonyesha: Uende mpaka nchi nitakayokuonyesha(m.1). 3.Mungu alimwahidi atakuwa taifa kubwa, lakini hakuwa na mtoto hata mmoja (ling. 11:30,Sarai alikuwa tasa, hakuwa na mtoto)! Lakini Abramu alikuwa na utii. Alimwamini Mungu kwa moyo. Rudia ilivyoandikwa katika m.4 na 7-8:Basi Abramu akaenda, kama Bwana alivyomwamuru… nao wakaingia katika nchi ya Kanaani. … Bwana akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu Bwana aliyemtokea.Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; alikuwa na Betheli upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea Bwana madhabahu huko, akaliitia jina la Bwana.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga ...

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha