Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

SIKU 3 YA 28

Mtoto wa pili wa Nuhu aliitwa Hamu. Mwana wa nne wa Hamu aliitwa Kanaani. Ukoo wa Kanaani ulienea katika nchi iliyokuwa kati ya mto Yordani na Bahari ya Kati (taz. 10:15-20). Ndiyo sababu ya nchi hii kuitwa nchi ya Kanaani. Nchi hii ndiyo aliyopewa Abramu na Mungu (12:5-7,Wakaingia katika nchi ya Kanaani.Abramu akapita katikati ya nchi mpaka mahali patakatifu pa Shekemu; mpaka mwaloni wa More. Na Wakanaani siku zile walikaa katika nchi hiyo.Bwana akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii). Leo twaona hekima ya Abramu jinsi alivyoondoa ugomvi kati yake na Lutu. Mwa 12:4 lasema: Lutu akaenda pamoja naye. Je, haya yalikuwa mapenzi ya Mungu? Aliyeitwa na Mungu na kupewa nchi ni Abramu,si Lutu (m.14-15,Bwana akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo, upande wa kaskazini, na wa kusini na wa mashariki na wa magharibi;maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele)!

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga ...

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha