Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

SIKU 7 YA 28

Watu wanaomtegemea Mungu kweli, wakiomba, hakika Mungu huwapatia haja zao. Kuna wakati watu hutucheka na kutuona kama tusiojibiwa. Au sisi wenyewe tunaweza kudhani Mungu hatusikii. Tena kuna nyakati tunajibiwa kwa namna tofauti na tulichoomba. Lakini Bwana atasikia nimwitapo. Ndio ushuhuda wa Mtunga zaburi (m.3). Kwa hiyo tusikate tamaa. Tumgojee Mungu (m.5, kumtumaini Bwana). Kisha tuombapo tuangalie vema baraka tulizokirimiwa. Zaburi inataja zipi? Rudia m.7-8, Umenitia furaha moyoni mwangu, Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai.Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, Bwana, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama. Hizi zaweza kuwa tayari ni majibu kwetu pia.

Andiko

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga ...

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha