Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

SIKU 8 YA 28

Abramu alipewa neno la faraja na la baraka nyingi: Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana(m.1). Ni neno la Mungu aliye juu sana, Muumba wa mbingu na nchi! Hata hivyo Abramu hakufurahi, maana hakuwa na mtoto. Akawa na mashaka juu ya ahadi ya Mungu. Je, uzao wake kweli utairithi nchi? Ndipo Mungu akaithibitisha tena ahadi yake,[Eliezeri] hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi. Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako(m.4-5)! Zingatia matokeo ya Abramu kusikiliza ahadi hiyo: Abramu akamwamini Bwana.Kwa hiyo habari inaendelea, Naye [Bwana]akamhesabia jambo hili kuwa haki(m.6)! Sikia Injili tena na tena ili udumu katika imani (ling. Rum 10:17,Imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo)!

siku 7siku 9

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga ...

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha