Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

SIKU 28 YA 28

Daudi anamsifu Mungu kwa ajili ya uumbaji wake, akionyesha jinsi jua, mwezi, nyota na viumbe vingine kama watu wanyonge vinavyosifu ukuu wake. Zab 8 imenukuliwa mara nyingi katika AJ. Yesu mwenyewe na Wakristo wa kwanza waliisoma kama unabii juu ya Kristo. Yesu akawaambia [wakuu wa makuhani na waandishi], Naam; hamkupata kusoma, Kwa vinywa vya watoto wachanga na wanyonyao umekamilisha sifa?Na katika Ebr 2:5-9 unaweza kusoma jinsi Wakristo wa kwanza walivyoelewa Zab 8. Ukuu wa binadamu unashuhudiwa, kwa sababu Mwana wa Mungu atakuwa ndugu yetu. Kama mwakilishi wa binadamu wote, Yesu atapewa mamlaka kamili juu ya uumbaji wote na kutimiza kikamilifu unabii wote wa Zab 8 (Efe 1:20-22 inathibitisha kwamba ndivyo ilivyotokea: Mungualipomfufua [Kristo]katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa).

Andiko

siku 27

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga ...

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha