Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

SIKU 5 YA 28

Bila shaka ni Mungualiyempa Abramu ushindi katika vita hii, maana alikwenda na watu wachache tu ili kupigana na adui mkubwa (m.14,Abramu aliposikia ya kwamba nduguye ametekwa mateka, akawapa silaha vijana wake, waliozaliwa katika nyumba yake, watu mia tatu na kumi na wanane). Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako(m.20)! Abramu aitwa "Mwebrania", maana ni mwana wa "Eberi", babu yake (habari za ukoo zinapatikana katika 11:14-26). Baadaye hata Waisraeli wakaitwa Waebrania. Abramu hakutaka kujenga uhusiano na watu wa Sodoma, maana ni waovu sana (13:13,Watu wa Sodoma walikuwa wabaya, wenye kufanya dhambi nyingi sana juu ya Bwana). Aliwasaidia tu kwa sababu ya Lutu. Kwa hiyo alimwambia mfalme wa Sodoma, Sitatwaa uzi wala gidamu ya kiatu wala cho chote kilicho chako(m.23). Je, unajijenga kwa waovu?

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga ...

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha