Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

SIKU 4 YA 28

Nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele. Na uzao wako nitaufanya uwe kama mavumbi ya nchi(m.15-16). Mungu alimhakikishia Abramu kuwa yeye ndiye aliyechaguliwa kati ya wanadamu wote. Na taifa litakalotoka katika uzao wake litakuwa taifa teule kati ya mataifa yote (12:2-3, Nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako)! Uchaguzi huu wa Mungu, je, sio ubaguzi? Ni kweli, inaonekana hivyo, lakini sivyo. Mpango wa Mungu ni wa ajabu: Na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa(12:3). Yesu Kristo ameutimiza! Kama Petro alivyoeleza katika Mdo 3:25-26,Ninyi mmekuwa watoto wa manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu aliagana na baba zenu, akimwambia Ibrahimu, Katika uzao wako kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa.Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga ...

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha