Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

SIKU 9 YA 28

Ili kuimarishwa zaidi katika imani, Abramu alitafuta uhakika zaidi kwa Mungu(m.8, Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, nipateje kujua ya kwamba nitairithi?). Tendo la kupasua wanyama vipande viwili lilitumika watu wawili au makundi mawili wakitaka kupatana kitu fulani. Ilibidi wote wawili wapite kati ya vipande vile vilivyoelekeana. Hivyo hufanya agano (mapatano, ling. Yer 34:18-20,Watu hao waliolivunja agano langu, wasioyatimiza maneno ya agano lile, walilolifanya mbele zangu, wakati ule walipomkata ndama vipande viwili, wakapita katikati ya vipande vile;wakuu wa Yuda, na wakuu wa Yerusalemu, matowashi, na makuhani, na watu wote wa nchi, waliopita katikati ya vipande vile vya huyo ndama;mimi nitawatia katika mikono ya adui zao, na katika mikono ya watu wale wanaowatafuta roho zao, na mizoga yao itakuwa ni chakula cha ndege za mbinguni, na cha wanyama wakali wa nchi). Mungu na Abramu hawalingani. Ni Mungu peke yake aliyepita kati ya vipande (m.17,Ikawa, jua lilipokuchwa likawa giza, tazama, tanuru ya moshi na mwenge unaowaka ulipita kati ya vile vipande vya nyama). Abramu hakuahidi lo lote. Mungu tu alitoa ahadi. Alifanya tendo la neema kwa ajili ya Abramu!

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga ...

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha