Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

SIKU 2 YA 28

Abramu ni chanzo cha taifa la Israeli. Katika historia ya Waisraeli nchi ya Misri ina nafasi muhimu. Fikiria Yusufu, Yakobo, Musa na hata Yesu mwenyewe alipokuwa mtoto mchanga, wote walifika Misri. Leo twaona Abramu alikimbilia huko kwa sababu ya njaa (m.10,Abramu akashuka Misri, akae huko kwa muda maana njaa ilikuwa nzito katika nchi). Badala ya kutegemea ulinzi wa Mungu, alifanya mbinu zake mwenyewe (m.11-13,Ikawa alipokuwa karibu kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, Tazama, najua ya kuwa u mwanamke mzuri wa uso;basi itakuwa, Wamisri watakapokuona watasema, Huyu ni mkewe; kisha wataniua mimi na wewe watakuacha hai.Tafadhali useme, wewe u ndugu yangu, iwe heri kwangu kwa ajili yako, na nafsi yangu iishi kwa ajili yako). Lakini mpango wake haukuwa na kibali cha Mungu. Mapigo ya Bwana yakaja juu ya nyumba ya Farao (m.17,Bwana akampiga Farao na nyumba yake mapigo makuu, kwa ajili ya Sarai, mkewe Abramu).  Abramu alikuwa kama sisi! Si mkamilifu.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga ...

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha