Soma Biblia Kila Siku 11/2024Sample

Wanafunzi wamemkubali Yesu awe namba 1 katika maisha yao wala si pesa au mali. Bila shaka wako pia Wakristo wengi Tanzania ambao wamekubali kujinyima raha fulani ya dunia kwa ajili ya jina la Yesu.Tutapata nini basi(m.27)?Yesu anathibitisha kwamba kweli watapata kitu, tena kitu kikubwa mno: Uraia wa ufalme wa Mungu na utawala pamoja na Yesu! Cheo hiki hakitaonekana sana katika ulimwengu huu. Lakini kitadhihirishwa wazi Yesu atakapoumba ulimwengu mpya! Tafakari Paulo anavyokaza kwamba katika maisha haya Mkristo huteswa pamoja na Yesu, lakini katika ulimwengu mpya tutashiriki utukufu wake:Kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.... Ni neno la kuaminiwa. Kwa maana, Kama tukifa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia; Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi(Rum 8:17 na 2 Tim 2:11-12).
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 11/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na moja pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Related Plans

God's Book: An Honest Look at the Bible's Toughest Topics

30 Powerful Prayers for Your Child Every Day This School Year

You Say You Believe, but Do You Obey?

Rebuilt Faith

24 Days to Reflect on God's Heart for Redemption

Game Changers: Devotions for Families Who Play Different (Age 8-12)

Awakening Faith: Hope From the Global Church

Protocols, Postures and Power of Thanksgiving

Sharing Your Faith in the Workplace
