YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 11/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 11/2024

DAY 10 OF 30

Leo jambo kuu ni hili: kuingia Mbinguni ni kwa neema tu. Ujira wetu, yaani uzima wa milele, ni uleule mmoja kwa wote, na hautolewi kutokana na ustahili wetu, bali kwa sababu Mungu ni mwema. Wanafunzi waliuliza,Tutapata nini basi(19:27)?Kwa hadithi hii Yesu anatuonya kwamba hata kama tumemtumikia kwa miaka mingi kwa uaminifu tusiwe tunaanza kujivuna na kufikiri tunastahili kuliko wengine. Tusiwaonee wivu waliochelewa kumpokea Yesu, bali tufurahi kwa sababu sisi wenyewe tumeokolewa:Msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni! (Lk 10:20)

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 11/2024

Soma Biblia Kila Siku 11/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na moja pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More