Soma Biblia Kila Siku 11/2024Sample

Hutokea watu wa Mungu wanapata shida pamoja na kwamba wanaendelea kumpenda na kumheshimu Mungu. Wakati mwingine Mungu mwenyewe anaruhusu mateso yatokee kama ilivyokuwa kwa Ayubu:Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu. ... Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. ... Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe(Ayubu 1:1, 8, 12). Mateso aliyopata Ayubu yalikuwa na kibali cha Mungu. Kadhalika katika zaburi hii, ila mtunzi anamlilia Mungu kuwa mbona amemwacha. Pia Mungu ameruhusu maadui zake wamwaibishe na kumfanya mtumwa wao. Mtunzi haoni sababu ya mateso hayo, lakini akitegemea Mungu yu pamoja naye anaendelea kumlilia,Amka, Bwana, mbona umelala? Ondoka, usitutupe kabisa. Mbona unatuficha uso wako, Na kusahau kuonewa na kudhulumiwa kwetu? Maana nafsi yetu imeinama mavumbini, Tumbo letu limegandamana na nchi. Uondoke, uwe msaada wetu, Utukomboe kwa ajili ya fadhili zako(m.23-26).
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 11/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na moja pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Related Plans

God's Book: An Honest Look at the Bible's Toughest Topics

30 Powerful Prayers for Your Child Every Day This School Year

You Say You Believe, but Do You Obey?

Rebuilt Faith

24 Days to Reflect on God's Heart for Redemption

Game Changers: Devotions for Families Who Play Different (Age 8-12)

Awakening Faith: Hope From the Global Church

Protocols, Postures and Power of Thanksgiving

Sharing Your Faith in the Workplace
