YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 11/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 11/2024

DAY 12 OF 30

Waliposikia ya kwamba Yesu anapita, walipaza sauti(m.30). Bila shaka hao vipofu walikuwa wameisikia habari yake. Na waliyosikia yalizaa imani na tumani mioyoni mwao. Sasa siku hiyo ghafula Yesu alikuwa anapatikana. Mara wakamwita, wala hawakujali maneno ya watu, bali walizidi kumwita hadi aliposimama. Na Yesu kweli aliwahurumia, na tangu siku ile wakawa wafuasi wake. Habari hiyo itukumbushe kutokusema ‘kesho’, Yesu anapotuita, balimtafuteni Bwana maadamu anapatikana, mwiteni, maadamu yu karibu(Isa 55:6-7). Je, baada ya kusaidiwa na Yesu ukawa mfuasi wake?

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 11/2024

Soma Biblia Kila Siku 11/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na moja pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More