YouVersion Logo
Search Icon

Somabiblia Kila Siku 3Sample

Somabiblia Kila Siku 3

DAY 5 OF 31

Mariamu alionyesha upendo wake mkubwa kwa Yesu kwa kumpaka marhamu (= manukato au uturi). Ni kitu kilichotoa harufu nzuri. Alimpaka kwa wingi maana ratli ni sawa na nusu lita. Thamani yake ilikuwa kubwa sana (denari 300). Denari moja ilikuwa sawa na malipo ya kibarua ya siku moja! Pia alimpaka Yesu kichwani (Mt 26:6-13). Leo twaweza kuonyesha upendo wetu kwa Yesu kwa kutoa mali au fedha zetu kwa kazi ya Injili, na pia kwa kuwasaidia wenye shida!

Scripture