YouVersion Logo
Search Icon

Somabiblia Kila Siku 3Sample

Somabiblia Kila Siku 3

DAY 31 OF 31

Watu wa Mungu hukuta dharau. Kwa nini? Tukijaribu kuelewa hali hii, tunaona jambo linalofanana nayo katika Ebr 12:3 kuhusu Bwana wetu: Mtafakarini sana yeye aliyestahimili mapingamizi makuu … msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu. Wakati watumwa wanapomtazama bwana wao kwa woga wa adhabu, waumini wa BWANA wanamtumaini kwa furaha. Tunatiwa moyo, tukikaza macho yetu kwa Yesu, mwanzilishi na mkamilishaji wa imani yetu. Basi, tumtumaini BWANA kwa umakini, na kungojea matendo yake.