YouVersion Logo
Search Icon

Somabiblia Kila Siku 3Sample

Somabiblia Kila Siku 3

DAY 4 OF 31

Kutokana na ishara za Yesu viongozi wa Wayahudi walifadhaika sana: Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini; na Warumi watakuja, watatuondolea mahali petu na taifa letu(m.47-48). Badala ya kunyenyekea na kumkubali Yesu walizidi kushikilia vyeo vyao kwa nguvu (m.49-50, 53 na 57). Kwa njia hiyo wao wenyewe walisababisha Warumi kuja kuharibu mji wao na taifa lao. [Yesu]alipofika karibu aliuona mji [wa Yerusalemu], akaulilia, akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako. Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako(Lk 19:41-44). Unabii huu wa Yesu ulitimizwa baada ya miaka kama 40, yaani mwaka 70 b.K. Zingatia m.52. Ni kwa mataifa yote!

Scripture