YouVersion Logo
Search Icon

Somabiblia Kila Siku 3Sample

Somabiblia Kila Siku 3

DAY 10 OF 31

Zaburi 120-134 hujulikana kama Nyimbo za wakweao, kwa kuwa ziliimbwa wakati wa kwenda Yerusalemu kwa sherehe kubwa za mwaka. Zaburi ni kilio cha mtu aliyechoka kwa uonevu. Anaishi mbali, tena kati ya watu wenye tabia ya kufanya vita. Uongo na hila zao ni kama mishale inayomchoma nafsini. Kwa hiyo anatamani kufika Yerusalemu, mahali pa amani. Je, katika shida zako humkimbilia nani? Mungu ndiye kimbilio letu. Amani yetu iko kwa Yesu. Tumtwike yeye fadhaa zetu zote(1 Pet 5:7).