YouVersion Logo
Search Icon

Somabiblia Kila Siku 3Sample

Somabiblia Kila Siku 3

DAY 7 OF 31

Ni ajabu sana kwamba njia ya Yesu kutukuzwa ni kifo cha msalaba(m.23-24; 27-28; 32-34)! Ni ajabu maana kifo cha msalaba kilikuwa cha aibu kabisa. Kwanza, ni wahalifu wabaya waliohukumiwa hivyo. Pili, walisulibiwa wakiwa karibu uchi. Tatu, mateso yao yalikuwa makali sana kupita njia nyingine za kuhukumiwa kifo. Siriya Yesu alivyofanya ni upendona utii. [Yesu] hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba(Flp 2:6-8). Alikufa badala yawengine akitimiza mapenziya Baba yake! Je, umeuona utukufu wake? Yohana akasema kuhusu Yesu, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! (Yn 1:29).

Scripture