YouVersion Logo
Search Icon

Somabiblia Kila Siku 3Sample

Somabiblia Kila Siku 3

DAY 9 OF 31

Wayahudi walitumia viatu vilivyokuwa wazi. Kwa hiyo wakiwa safarini, miguu yao ilichafuka kwa urahisi. Walikuwa na desturi ya kutawadha (kunawa) miguu wakijiandaa kula. Hawakukalia viti wakati wa kula bali walikaa chini kwenye sakafu. Kwa hiyo ilikuwa muhimu zaidi kuwa na miguu safi. Yesu akijua kwamba karibuni atarudi kwa Baba, alitenda tendo hili la pekee ili kuwaonyesha kwamba aliwapenda upeo(m.1; 3-5). Pia aliwapa wanafunzi wake kielelezo (m.12-16). Heri ninyi mkiyatenda (m.17)!

Scripture