YouVersion Logo
Search Icon

Somabiblia Kila Siku 3Sample

Somabiblia Kila Siku 3

DAY 8 OF 31

Mungu ndiye aliyewafanya Wayahudi wengi kuwa na mioyo migumu: Amewapofusha macho, Ameifanya mizito mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao ...(m.40). Aliyotabiri nabii Isaya yakatimizwa. Na wale viongozi walioamini hawakukiri kwa wazi: Kwa maana walipenda utukufu wa wanadamu kuliko utukufu wa Mungu (m.42f). Lakini mtu anayetaka kuwa mfuasi wa Yesu kwa siri, yuko hatarini kupoteza imani yake (ling. Mt 10:32-33: Kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni. Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni). Je, kwako ni muhimu zaidi kupata sifa kwa nani?

Scripture