YouVersion Logo
Search Icon

Somabiblia Kila Siku 3Sample

Somabiblia Kila Siku 3

DAY 3 OF 31

Leo tumepewa kutafakari miisho ya watu wa aina mbili: mtu mnyofu na mtu mwovu. Mtu mnyofu hujiepusha na uovu na hutafuta kutenda mema. Kwa upande mwingine, mtu mwovu hutafuta kumwangamiza mtu mnyofu. Je, miisho yao ni nini? Umtazame mtu mnyofu, maana mwisho wake huyo mtu ni amani. Wasio haki mwisho waowataharibiwa. Wokovu wa wenye haki una Bwana(m.37-39). Kuifuata njia ya haki na kumngoja Bwana kuna faida ya kudumu katika maisha haya na hata milele.