YouVersion Logo
Search Icon

Somabiblia Kila Siku 3Sample

Somabiblia Kila Siku 3

DAY 2 OF 31

Yesu alipoiona huzuni ya Mariamu na wale waliokuja kumfariji akaugua rohoni mwake akalia machozi (m.33-36)! Akamwomba Baba yake amfufue Lazaro (m.41-42). Akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi ... (m.43-44). Ajabu sana, sivyo? Aliyetenda haya ni NENO ambaye kwa yeye vitu vyote vilifanyika: Hapo mwanzo kulikuwako Nneo, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika(Yn 1:1-3)! Kwa ishara hii Yesu alitukuzwa. Inathibitisha pia ukweli wa maneno yake aliyosema: Mimi ndimi ufufuo na uzima!

Scripture