YouVersion Logo
Search Icon

Somabiblia Kila Siku 3Sample

Somabiblia Kila Siku 3

DAY 15 OF 31

Yesu amefundisha kwamba kulishika neno lake ni dalili ya kumpenda (14:23-24). Wakati Yesu alipokuwa anasisitiza hivyo, maneno yake yalikuwa bado hayajaandikwa. Swali linakuja: Neno la Yesu ni lipi? Ni lipi lile neno tunalotakiwa kulishika? Katika somo la leo Yesu hutupa jibu la swali hili:huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu ... atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia(m.26). Katika maandiko ya Mitume (Agano Jipya) twaona jinsi Yesu alivyoitimiza ahadi aliyowapa!

Scripture