YouVersion Logo
Search Icon

Somabiblia Kila Siku 3Sample

Somabiblia Kila Siku 3

DAY 18 OF 31

Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe(m.11). Furaha ni jambo muhimu na la msingi katika Ukristo! Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini(Flp 4:4). Itakuwaje furaha ya Yesu kuwa ndani yetu? 1.Kwa kuutambua upendo wake kwetu na kuupokea (m.9 na 12-13). 2.Kwa kuzitii amri zake na kuzifuata (m.10). Ni amri kama hii: Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi(m.12 na 17). Tukishapokea upendo wake, yaani wokovu wake, twapata moyo mpya unaompenda Yesu na amri zake.

Scripture