YouVersion Logo
Search Icon

Somabiblia Kila Siku 3Sample

Somabiblia Kila Siku 3

DAY 14 OF 31

Tukitaka kupata kitu kwa mtu mkubwa, mara nyingi inasaidia tukimpitia mtu ambaye yupo karibu na huyo mkubwa. Leo Yesu anatufundisha kwamba ndivyo ilivyo kwa Mungu. Lazima tumwendee Mungu Mtakatifu kwa kumpitia Mwana wake, yaani, Yesu Kristo, Mpatanishi wetu (m.12-14)! Yesu ni mwombeziwetu kwa Mungu Baba. Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote(1 Yoh 2:1-2). Kwa hiyo omba kwa jina la Yesu, yaani, omba ukimtegemea yeye! Mfuasi wa Yesu afanyaye hivyo huambiwa na Yesu: kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya (m.12).

Scripture