YouVersion Logo
Search Icon

Somabiblia Kila Siku 3Sample

Somabiblia Kila Siku 3

DAY 19 OF 31

Yesu alifundisha wazi kwamba katika kumfuata yeye, pia kuna mambo magumu. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu ... kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia(m.19). Ndivyo inavyotokea k.m. mtu akiokoka na kuachana na pombe. Inawezekana kabisa kwamba waliozoea kushiriki naye kilabuni watamchukia na kumwudhi kutokana na msimamo wake mpya. Hali hiyo ni msalaba kwa Mkristo, na majaribu. Yesu anasema, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona(Mt 16:24-25).

Scripture